Man city yaua 4-0, Aguero apiga Hat trick


Timu ya Manchester city imeondoka na pointi kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Borrusia Moenchengladbach.

Mshambuliaji wa Manchester city Sergio Aguero alifunga mabao 3 peke yake kwenye dakika ya 9, 28 na 77 huku lile la mwisho likiwekwa nyavuni na Kelechi Ihenacho aliyefunga dakika ya 90.

Manchester city sasa inaungana na Barcelona yenye pointi tatu baada ya jana kupata ushindi wa bao 7-0 dhidi ya Celtic kwenye kundi hilo.

Comments