Man utd yatoa gundu ikipata ushindi wa bao 3-1, sasa kuivaa city uso kwa uso EFL


Baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo jana Manchester united imetoa gundu baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-1 katika mechi ya kombe la ligi (EFL).

Man utd ambayo imefuzu kuelekea raundi ya 4 ya mshindano hayo itavaana uso kwa uso na Manchester city ambayo jana iliweza kuindoa Swansea baada ya kutoka na ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Liberty.

Ratiba hiyo inampa nafasi Jose Mourinho nafasi nyingine ya kulipiza kisasi baada ya kupoteza mechi ya kwanza katika uwanja wa Old Trafford.

Kwa mara nyingine tena Manchester united inapata nafasi ya kutumia uwanja wake wa nyumbani ambapo city itakuwa mgeni wa mashetani hao wekundu kwa mara ya pili baada ya ule mchezo wa ligi ambao city alipata ushindi wa bao 2-1.

Comments