Timu ya Simba imeanza Vizuri kwenye uwanja wa Uhuru baada ya kuifunga Ruvu Shooting kwa ushindo wa bao 2-1.
Ruvu Shooting ilpata bao la kuongoza dakika ya 8 kupita Abrahiman ambaye alifunga baada Angban kutoka kwenye goli lake.
Hata hivyo Simba ilijipanga vizuri na iliweza kupata bao la kuchomoa kupitia Ibrahim Ajib aliyefunga dakika ya 21 baada ya kuunganisha vizuri krosi ya Mohamedi Hussein huku Laudit Mavugo akifunga lile la ushindi kwenye dakika ya 50.
Pia katika mechi nyingine timu ya Azam imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, bao pekee la ushindi likiwa limefungwa na Michael Balour.

Comments
Post a Comment