Mbao FC yamziba mdomo Masau bwire, yaichapa Ruvu Shooting 4-1.


Msemaji wa timu ya Ruvu Shooting huenda akawa akakosa kauli baada ya Ruvu Shooting kupokea kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa mbao FC.

Kabla ya mechi ya Simba na Ruvu Shooting, Masau Bwire alikuwa kwenye vita nzito ya maneno dhidi ya Simba lakini hata hivyo timu yake ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na wana msimbazi hao.

Mbao FC ya shinyanga leo imefanya kweli baada ya kupokea vipigo viwili mfululizo kutoka kwa Mbeya city na African Lyon.

Kwa matokeo hayo timu ya Mbao sasa inakusanya jumla ya pointi 4, tangu kuanza kwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara maarufu kama VPL.

Comments