Timu ya Mbeya leo itashuka katika uwanja CCM Kirumba mkoani Mwanza katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC.
Msemaji wa Mbeya city Dismas Ten amesema kuwa katika mechi hiyo hawaweki dhamana ya ushindi moja kwa moja kwa kuwa lolote linaweza kutokea kwenye mpira.
"Ni vigumu kusema kuwa tutapata ushindi, mpira ni mchezo wa dakika 90 hivyo lolote linaweza kutokea." Alisema Dismas.
Katika mechi nyingine Kagera Sugar itaikaribisha Mwadui ya Shinyanga ikiwa ni kwa mara ya Kagera sugar inazindua uwanja huo baada ya kufanyiwa marekebisho ya kuwekewa nyasi bandia.

Comments
Post a Comment