Msemaji wa timu ya Mbeya city Dismas Temu amesema kuwa timu hiyo ipo kamili kuikabili Mbeya city kwenye mchezo wa ligi kuu kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza kuhusiana na maandalizi Temu alisema kuwa timu yao imejiandaa vizuri na wamewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuongeza hamasa ushindi kwa Mbeya city.
"Tunashuruku timu yetu ipo juu kwenye msimamo, kikubwa tunahitaji kushinda mchezo wa kesho na kuondoka na pointi 3, Mbeya city imebadilika siyo ile ya msimu uliopita hivyo tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi siku ya kesho." Alisema Temu
Mbeya itashuka dimbani kesho ikimkosa mchezaji wake Geofrey Mbao ambaye alipatwa na majeraha katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Toto Africa Mwanza.
Comments
Post a Comment