Mechi ya Azam na Simba ni kitendawili uwanja wa Uhuru


Ingawa jana TFF kupitia tovuti yake iliweka bayana kuwa mechi kati ya Simba na Azam itachezwa kwenye uwanja Uhuru, lakini bado zipo dalili za mashaka kulingana na kauli ya mkurugenzi mtendaji wa timu ya Azam.

Kauli ya TFF imesemwa kinyume na Mkurugenzi mtendaji wa timu ya Azam Saadi kaweka aliyeweka wazi bado wameshikilia msimamo wao wa kuwa mechi hiyo ichezwe katika uwanja wa Chamanzi Complex.

Azam ambayo jana ilikabidhiwa ngao halisi kutoka China bado hainoeshi kuridhia mpango huo wa TFF licha ya kukaa pamoja kwenye meza ya mazungumzo.

Kauli iliyotolewa na Saadi Kawemba haina tofauti na ile ya msemaji wa Azam Jaffar Idd ambaye jana alizungumza sawa sawa na bosi wake. Saadi aliweka wazi kuwa wapo tayari kucheza uwanja wa uhuru iwapo TFF watatengua ratiba yao na ionekane ni Simba v Azam ikiashiria kuwa Azam itakuwa ugenini kwa Simba na kuipisha TFF ijipange kuipeleka Simba Chamanzi katika mechi ya marudiano.

 Bado tupo njia panda ingawa tunafahamu kuwa TFF ndio msemaji wa mwisho, tunaomba kila kheri kuwepo na maelewano halisi baina ya timu ya Azam na TFF.

Comments