Messi arudi kwa kasi timu ya taifa


Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amerudi kwa kasi kwenye timu ya taifa baada ya jana kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya Uruguay na kuyafanya matokeo kuwa 1-0.

Awali mchezaji huyo alitangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kukosa ubingwa kwenye fainali michuano ya Copa America miezi miwili iliyopita.

Argentina bila Sergio Aguero ilikuwa salama chini ya Lionel Messi ambaye alifunga bao hilo la pekee kwenye dakika ya 43 ya mchezo huo, na kuonesha kiwango kiwango cha kwa muda wa dakika zote 90.

Comments