Washambuliaji nyota wanaowika barani Ulaya kwa sasa Lionel Messi na Antonio Griezman leo watakutana kwenye mtanange wa jioni kati ya Barcelona na Atletico Madrid katika uwanja wa Camp Nou leo.
Barcelona imeshinda mechi tatu na kupoteza moja lakini kwa upande wa Atletico Madrid yenyewe imshinda mechi mbili na kutoa sare mechi.
Messi na Griezman wote kwa pamoja wameshachungulia nyavuni katika mechi hizo walizocheza hadi sasa huku kila mmoja akiwa amechungulia nyavuni mara nne mpaka sasa.
Kuna uwezekano mkubwa kila mmoja akapata bao siku ya leo ingawa timu itakayotengeneza nafasi nyingi inaweza kupata magoli mengi na kuondoka na pointi 3 siku ya leo.
Barceona ilipata ushindi mnono katika mechi ya mwisho na hali kadhalika kwa Atletico Madrdid pia hivyo timu zote leo zina morali ya hali juu, huenda kukawa na mchezo mzuri wa kuvutia na wenye ushindani wa hali juu siku ya leo.

Comments
Post a Comment