Kocha wa sasa wa Kagera Sugar Mecky Mexime anakutana uso kwa uso na timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar katika mechi ya ligi kuu wikiendi hii.
Mexime ambaye mwaka jana alikuwa akiiona Mtibwa Sugar amesema hakutakuwa na urafiki kwenye mchezo huo matarajio yake makubwa ni kuifunga Mtibwa ili kuondoka na pointi 3 kwenye uwanja wa Manungu.
"Matarajio yangu ni ushindi, kuhama ni jambo la kawaida pamoja na yote mimi si kocha wa kwanza kuhama lakini kwa sasa nafikiria ushindi kwanza." Alisema Mexime.
Mbali na kuiona Mtibwa Mexime amewahi kuwatumikia wakata miwa hao wa Morogoro kwa mafanikio na kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu mwaka 1996 na mwaka 2000.

Comments
Post a Comment