Mkhitaryan kuikosa Europe ligi kesho, Rashford aingia mazoezini


Kiungo mshambuliaji wa Manchester united Henrikh Mkhitaryan ameshindwa kuambatana na kikosi cha Manchester united mazoezini kutokana na majeraha ya goti yanayomkabili.

Mkhitaryan anaungana na beki Phil Jones ambao kwa pamoja watashindwa kucheza mechi ya kesho dhidi ya Feyernood ya Uholanzi.

Kocha wa Manchester united Jose Mourinho ameweka wazi kuwa mshambuliaji kinda Marcus Rashford ataungana pamoja na Zlatan Ibrahimovic na Wayne kuongoza safu ya ushambuliaji.

Rashford ambaye alirudisha uhai kwenye kikosi cha Manchester united katika mechi dhidi ya Manchester city ameungana na wachezaji wenzake kwnenye mazoezi ya mwisho ya kujiandaa na mechi hiyo ya Europa ligi hapo kesho.

Comments