Mkwara wa Masau Bwire kwa Simba ni hatari.


Msemaji wa timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amesema kuwa Simba wa sasa hatishi hivyo wataingia uwanja wa Uhuru kwa malengo ya kutoka na pointi tatu .

Akizungumza kwa kujiamini msemaji huyo alitamba kuwa ni rahisi kumfukuza Simba wa sasa kwa vikobo huku akisisitiza kuwa timu hiyo haina makali.

"Ni wazi tumejipanga, nadhani bakora inamtosha Simba, kwa sasa wapo wanyama wa wakali wanaotisha kuliko Simba msituni." Alisema Msemaji huyo

Kwa upande wa Haji Manara ambaye ni msemaji wa Simba alisema kuwa wanaamini Simba itaibuka na ushindi kwa kuwa Ruvu Shooting bado ni timu ndogo kwa wana Msimbai hao.

Comments