Msikie pluijm eti stand utd ni wagumu kuliko Simba


Kocha wa Yanga Hans Pluijm amesema kuwa mechi yao watani wa jadi Simba ni nyepesi kulinganisha na ile waliypoteza dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Kambarage.

Yanga ilipoteza pointi 3 baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Stand huku watani wao wa Simba wakitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji.

Katika mechi nne za mwisho kati ya Simba na Yanga, Simba imepoteza mbili, imeota sare mechi moja na kushinda mechi hivyo kocha wa Yanga ana imani kuwa pointi 3 kutoka kwa Simba ziko palepale.

"Nadhani sina cha kuhofia naisubiri kwa hamu siku ya Octoba 1 najua ushindi ni wetu, tulikuwa na wakati mgumu tulipocheza na Stand united lakini kwa Simba ni rahisi kuliko Shinyanga." Alisema Hans


Comments