MSN yazidi kufanya balaa, Barca ikiua 5-1


Utatu wa timu ya Barcelona maarufu kama MSN umeendeleza ubabe kwenye ligi ya Hispania baada ya kushusha kichapo cha mabao 5-1 nyumbani kwa Leganes.

Messi alianza kufungua ukurusa wa mabao dakika ya 15, Suarez alifunga la bao la pili dakika ya 31, Neymar alifunga bao la tatu dakika ya 44, Messi kwa mara nyingine alifunga dakika ya 55  kwa mkwaju wa penati na Rafinha alifunga bao la 5.

Kabla ya mechi ya leo nyota wa Barcelona akiwemo Lionel Messi waliomba radhi kwa mashabiki wao baada ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Alaves katika uwanja wa Camp Nou.

Comments