Mtibwa yatamba kuisambaratisha Maji maji ya Songea


Timu ya Mtibwa Sugar ambayo leo itacheza mechi ya ligi katika uwanja wa manungu imetamba kuondoka na pointi mbele ya Maji maji ya Songea.

Akizungumza na mwandishi wetu msemaji wa timu ya Mtibwa Tobias Kifaru amesema kuwa mechi ya leo ni sehemu ya kulipiza kisasi kwao baada ya kufungwa na timu hiyo.

"Leo tumejiandaa kuondoka na pointi tatu ni lazima tushinde, tunaenda kulipa kisasi dhidi ya Maji maji ambao wao walitufunga mara ya mara ya mwisho." Alisema kifaru

Kwa upande wa maandalizi msemaji huyo alisema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mechi hiyo kutoka na hali nzuri waliyokuwanayo mazoezin.

Comments