Timu ya Ndanda FC ya Mtwara jana iliangukia pua katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mbao FC.
Mshambulaiji wa Mbao FC Venance Ludovic ndiye aliyeibuka shujaa kwenye mechi hiyo baada ya kutupia nyavuni bao zote mbili katika dakika ya 19 na 58 na kuhakikishia timu yake idadi ya pointi 3.
Matokeo hayo yanaifanya Mbao FC kubeba jumla ya pointi 7 katika msimamo wa ligi kuu ikirejesha upya matumaini yake baada ya kupokea kipigo kutoka kwa African Lyon pamoja na Mbeya City.

Comments
Post a Comment