Ndanda: Yanga hapati kitu kesho


Timu ya Ndanda imesema kuwa timu ya Yanga isitegemee matokeo ya ushindi watakapocheza na timu hiyo kesho kwenye mechi ya ligi kuu.

Ndanda ambayo imejuruhiwa mara mbili imesema kuwa wanataka kuionesha Yanga soka safi na kuhakikisha wanaondoka na pointi 3 katika uwanja wao wa nyumbani.

"Tunahitaji ushindi, tumepoteza mechi mbili bila shaka Yanga wategemee matokeo tofauti na ushindi." Alisema Idris ambaye ni msemaji wa timu hiyo

Pia katika uwanja wa taifa kutakuwepo na mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting ambayo itachezwa kesho majira ya saa 10 za jioni.

Comments