Timu ya Simba leo kwenye uwanja wa taifa imeondoka na pointi baada ya kuifunga Mtibwa Sugar bao 2-0.
Washambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib pamoja na Laudit Mavugo wameendelea na kazi ya kufumania nyavu baada ya kuipa Simba ushindi wa magoli hayo.
Ibrahim Ajib aliipatia Simba bao la kwanza dakika ya 53 ya mchezo na baadae Mavugo alipigilia msumari wa mwisho baada ya kufunga bao la pili dakika ya 67.
Kwenye mechi nyingine jijini Mbeya Tanzania Prisons katika uwanja Sokoine imeondoka na pointi 3 baada ya kuifunga bao 1-0 Toto Africa.
Comments
Post a Comment