Ni Mourinho v Gurdiola leo (OLD TRAFFORD)


Leo katika ligi ya England kutakuwa na mechi kali kati ya mahasimu wa jiji la Manchester katika uwanja wa Old Trafford ambapo Man united itaikaribisha city nyumbani.

Ikumbukwe mbali na upinzani uliopo baina ya timu hizo, pia kuna upinzani mkali baina ya makocha hao ambao walikuwa hawaelewani tangu walipokuwa kwenye ligi ya Hispania.

Kwa mara ya kwanza makocha hao wakiwa wapya kwenye timu zao wanakutana katika ligi ya England leo baada ya upinzani mkali waliokuwa nao wakati Gurdiola akiwa kocha wa Barcelona na Mourinho akiwa kocha wa Real Madrid.

Mbali na Gurdiola kumkosa Sergio Aguero kwenye mechi ya leo kwa upande wake amesisitiza kuwa atashambulia kama ilivyo kawaida katika timu zote alizofundisha ikiwemo Barcelona na Bayern Munich huku kwa upande wa Mourinho tukisubiri atakuja na mbwembwe zipi siku ya leo.

Nina imani kuna mvuto wa aina yake kwenye mechi hii ambayo itachezwa mapema leo majira ya saa 8.30 za mchana kwa saa za Afrika za Mashariki.

Comments