Kocha wa timu ya Simba Joseph Omog bado ameendelea kutilia mkazo suala kufumania nyavu kwa washambuliaji wake Ludit Mavugo, Fredrick Blagnon pamoja na Ame Ali.
Omog ameendelea kutilia mkazo suala ufungaji kwa washambuliaji wake ambao walikuwa wakiwa mbinu mbadala na kocha huyo.
Kuelekea mchezo wa watani wa jadi Octoba 1 kocha huyo amewataka washambuliaji wake kutumia vizuri nafasi wanazopata pindi wanapofika kwenye lango la timu pinzani.
Kocha aliongeza kuwa kumekuwa na makosa kadhaa kwa washambuliaji ambao kuna wakati hushindwa kupasia nyavu wakiwa wao na goli.
Comments
Post a Comment