Kocha wa Yanga Hans Der Pluijm amesema kuwa endapo Mrisho atajiunga tena na timu hiyo atakuwa na wakati mgumu kupata namba kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kuwepo kwa wachezaji wenye kiwango cha hali ya juu kuliko yeye.
Hivi karibuni Ngassa alivunja mkataba wake na Free State ambayo ndiyo timu aliyokuwa akiitumikia nchini Afrika Kusini na hivyo anahusishwa kurejea tena Yanga kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Novemba mwaka huu.
Pluijm alisisitiza kuwa kwa sasa timu hiyo ina wachezaji wanne wakali ambao wanacheza kwenye nafasi ya Ngassa ambao kwa umri ni wadogo na wana kasi ya hali ya juu uwanjani .
"Nadhani tutampokea kutokana na heshima aliyonayo kwenye timu hii, kwenye suala la kupata namba inabidi aongeze juhudi kubwa." Alisema kocha huyo

Comments
Post a Comment