Prisons yatamba kumkazia Azam kesho


Timu ya Prisons imesema kuwa ni lazima iondoke na pointi tatu katika uwanja wa Sokoine itakapocheza na timu ya Azam kesho.

Kocha msaidizi wa Prisons Shabani Kazumba amesema kuwa mechi iliyopita walikosa matokeo ya ushindi kutokana na kupata muda mdogo wa mazoezi ambapo sasa wamejipanga vema kwa ajili ya kuondoka na ushindi kesho.

"Tulishindwa kufanya vizuri kwenye mchezo uliopia kutokana na uchovu, hatukupata muda mwingi wa kujiandaa hivyo ni lazima tupate ushindi siku ya kesho." Alisema Kazumba

"Tunataka kureje juu ya msimamo wa ligi kuu hayo ndiyo malengo, ili kufika hapo tunahitaji kushinda, pointi 3 ni muhimu kwetu." Aliongeza kocha huyo


Comments