Ronaldo, Morata waibeba Madrid maji ya jioni, waikalisha Sporting CP 2-1


Washambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo pamoja na Alvaro Morata wameinyanyua timu hiyo baada ya kufunga magoli mawili yaliyopeleka pointi 3 Bernabeu.

Sporting CP ilipata bao dakika ya 48 kuongoza kwa muda wote, hadi pale Ronaldo alipochomoa bao la kwanza dakika ya 88 na Morata kuzamisha bao la ushindi dakika ya 90 kabla ya kumalizika kwa mpira.

Juhudi za washambuliaji zimeifanya Real Madrid kuondoka na pointi 3 baada ya kupata wakati mgumu kwa dakika 87.

Comments