Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti boys tayari imefanikiwa kutua Kigali Rwanda kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Congo.
Serengeti inaweka kambi yake nchini Rwanda kwa muda wa siku 10 ili kujiweka tayari kuondoka na ushindi itakapotua ugenini katika mechi ya marudiano baada ya kushinda ule wa nyumbani.
Serengeti ambayo ilishinda bao 3-2 nyumbani inasaka kwa udi na uvumba tiketi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa Afrika hii ikiwa ni nafasi pekee ya mwisho kupenya kwenye fainali hizo.
Vijana hao watashuka dimbani siku ya Octoba 2 mwaka huu katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa katika ardhi ya Congo Brazzaville.

Comments
Post a Comment