Mshabuliaji wa zamani wa Sunderland na West Brom Stephane Sessegnon amesaini miaka 2 katika timu ya Montpellier inashiriki ligi kuu ya Ufaransa (League 1).
Sessegnon alitemwa na West Brom mwishoni mwa msimu uliopita na kuwa mchezaji huru ambaye anaweza kufanya makubalino na timu yoyote inayomwitaji kama ilivyofanya Montpellier.
Sessegnon amewahi kuvunja rekodi ya usajili kwenye timu ya West Brom baada ya kusajili kwa dau la paundi 5.5 Milioni akitokea Sunderland mwaka 2013.
Hii si mara ya kwanza kwa Sessegnon kucheza nchini Ufaransa amewahi kufanya hivyo akiwa na Le Mans, Creteil pamoja na Paris St Germain (PSG).

Comments
Post a Comment