Siang'a afariki dunia, ni yule aliyeipeleka Simba makundi mwaka 2003


Kocha wa zamani wa timu ya Simba James Siang'a amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Kenya ndiye aliyeiongoza Simba kuing'oa Zamaleck ya Misri kwenye hatua ya 16 bora mwaka 2003 na kuiwezesha timu hiyo kuingia kwenye hatua ya makundi.

Pia kocha huyo amewahi kuzinoa Mtibwa Sugar na Moro united na baadae Express ya Uganda pamoja na Gor Mahia ya Kenya baada ya kuondoka Tanzania.

Comments