Simba, Lyon zapelekwa taifa


Timu ya Simba pamoja African Lyon zimerejeshwa kwenye uwanja wa taifa wa Benjamini mkapa kupisha baadhi ya marekebisho kwenye uwanja wa Uhuru.

Awali Simba ilituma barua ya maombi ya kurejea kwenye uwanja siku tatu zilizopita kutokana na mapungufu ya wazi yaliyopo kwenye uwanja wa uhuru ambao nyasi zake zimeshuka kiwango hali inayopelekea kuchunika kwa baadhi ya wachezaji.

TFF imefanya mabadiliko hayo kulingana na halisi ya uwanja wa Uhuru na sasa Simba katika mechi dhidi ya Majimaji siku ya jumamosi itarejea kwenye uwanja huo , pia African Lyon itatumia uwanja huo kwenye mechi dhidi Kagera Sugar siku ya jumatatu.

Pia uwanja huo utatumika siku ya jumapili ambapo wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wanaozisapoti timu za Simba na Yanga watacheza mechi siku ya jumapili kama sehemu ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani.

Comments