Simba yaendelea kufanya yao VPL, yailipua Majimaji 4-0


Timu ya Simba imeendelea na kasi yake ya ushindi ligi kuu baada ya kuibuka ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji ya Songea jana.

Simba ambayo ilionekana kutawala zaidi kipindi cha pili baada ya kuingia kwa Ibrahim Mohamed na Ame Ali ilipata mabao hayo kupitia Jamal Mnyate na Shiza kichuya ambao kila mmoja alifunga magoli 2.

Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuongoza kwenye msimamo wa ligi ambapo hadi sasa imekusanya idadi ya pointi zisizopungua 16 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 10 ambayo ina michezo miwili mkononi.

Baadhi ya Mechi za ligi kuu zitaendelea siku ya leo ambapo Yanga itakuwa mwenyeji wa Stand united katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Comments