Simba yaukingia kisogo uwanja wa Uhuru


Baada ya kucheza idadi ya mechi 3 kwenye uwanja wa Uhuru timu Simba imeandikia TFF barua ikiwataka kuwarudisha kwenye uwanja wa Uhuru kabla ya kucheza na Yanga.

Barua hiyo ya Simba ilifafanua kuwa nyasi za plastic zilizopo kwenye uwanja wa uhuru hazipo kwenye kiwango sahihi hali inayopekelea baadhi ya majeraha kwa baadhi ya wachezaji.

Katika Barua Simba ilionesha wazi nia yao ya kutumia uwanja huo kwa kuanza na mechi dhidi ya Majimaji ya Songea ambayo itachezwa wiki hii.

Mbali na maombi hayo ya Simba pia baadhi ya wachezaji akiwemo Nadir Haroub 'Cannavaro' wamewahi kutoa malalamiko kutokana na kiwango duni cha nyasi zinazotumika kwenye uwanja huo.

Comments