Baada ya mbwembwe za mtaani hatimaye Simba imedhihirisha ubora wake mbele ya Azam baada ya kuifunga timu hiyo bao 1-0 katika uwanja wa taifa.
Bao pekee la Simba liliwekwa nyavuni na Shiza kichuya aliyefunga kipindi cha pili dakika ya 76 ya mchezo huo na kuwanyanyua kidedea wababe hao wa msimbazi.
Kipindi cha kwanza Azam walionekana kuwazidi kidogo Simba kwenye eneo la kiungo lakin hata hivyo Simba ilirejea kwenye nguvu yake kipindi cha pili baada ya kuingia kwa Said Ndemla aliyejaza nguvu kwenye eneo la kiungo.
Ushindi wa Simba unaishusha Azam ambayo sasa inalingana pointi na Yanga ambayo imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui ya Shinyanga zote pamoja zikiwa na pointi 10 na Simba juu ya msimamo kwa pointi 13.

Comments
Post a Comment