Timu ya Tottenham imeshindwa kutamba nyumbani mbele ya Monaco ya Ufaransa baada ya jana kufungwa bao 2-1.
Monaco ilipata bao hizo kupitia Bernado Silva aliyefunga dakika ya 16 na Thomas Lemar aliyefunga bao la pili dakika ya 31 na bao pekee na la Spurs lilifungwa na Toby Alderweireld dakika 45 kabla ya filimbi ya mapumziko.
Spurs inatumia uwanja wa Wembley kwenye mechi zote za ligi ya mabingwa kama uwanja wake wa nyumbani lakini jana imeshindwa kuwika uwanjani hapo.

Comments
Post a Comment