Mbali na migogoro waliyonayo Stand united leo timu hiyo imeweza kuibuka na ushindi baada ya kuilaza Toto Africa bao 1-0 kwenye uwanja wa Kambarage.
Stand united ilipata bao hilo kupitia Adam Kingwande aliyefunga kwa mpira wa Adhabu kwenye dakika ya 39 ya mechi hiyo.
Akizungumzia furaha ya ushindi huo nahodha wa timu ya Stand united Jacob Massawe alisema amevutiwa na jinsi timu hiyo inavyocheza na kuisifu safu ya ulinzi ambayo inaongozwa chini yake kwa kutoruhusu bao ndani ya michezo mitatu sasa.
"Timu yetu iko vizuri, hakika napenda kuisifu safu ya ulinzi ya timu hii ambayo haijaruhusu bao lolote hadi sasa." Alisema Massawe
Kwa upande wa Salum Chuku ambaye ndiye nahodha wa Toto Africa alisema kuwa uwanja ndiyo chanzo cha matokeo mabaya waliopata kwenye mechi hiyo.
"Nadhani uwanja huu siyo, na ndiyo maana tumekosa matokeo mazuri siku ya leo." Alisema nahodha huyo.
Kwa matokeo hayo yanaifanya timu ya Stand united kujikusanyia jumla ya pointi 5 baada kutoa sare michezo miwili na kushinda mechi ya leo.

Comments
Post a Comment