Mashabiki wa Stand united ya Shinyanga pamoja na wale wa Simba jana ilikuwa siku yao kutokana na bingwa mtetezi Yanga kupokea kichapo cha bao 1-0 katika uwanja wa Kambarage.
Bao pekee la Pastory Athanas aliyefunga dakika ya 60 ndilo lililoilaza Yanga Kambarage na kuziacha pointi 3 zikienda kwa wapiga debe hao Shinyanga.
Yanga imepoteza mechi moja kati ya mechi 5 ilizocheza ikiwemo ile sare dhidi ya Ndanda FC hata hivyo timu hiyo bado ina mchezo mmoja mkononi dhidi ya JKT Ruvu.
Mbali na mechi zilizochezwa wikiendi bado mechi ligi kuu zinaendelea siku ya leo ambapo African Lyon itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa taifa.

Comments
Post a Comment