Suarez avunja rekodi ya CR7


Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez amevunja rekodi ya Christiano Ronaldo baada ya kuongoza kutoa pasi nyingi za mgoli ukijumlisha idadi ya magoli aliyofunga kwenye mechi mia moja za kwanza tangu aliposajiliwa Barcelona.

Mchanganyiko huo unamfanya Suarez kuwa kinara mbele ya Christiano Ronaldo pamoja na Lionel Messi akiwa na magoli 88 pamoja na pasi za magoli 43 jumla ya mchanganyiko huo ukiwa na idadi ya alama 131 sawa na asilimia 80.

Kwa upande wa Christiano Ronald amefunga jumla ya magoli ya 95, pasi za magoli 29 akiwa na idadi ya alama 124 sawa na asilimia 76, na kwa Lionel Messi alifunga magoli 41, pasi za magoli zikiwa 14 jumla idadi ni alama 55 sawa na asilimia 67.

Luis Suarez 29, ndiye anayesadikika kuwa mshambuliaji tishio kwa sasa ulimwenguni kutokana na uwezo wake wa kufumania nyavu akiwa na idadi ya magoli yasipongua 229 hadi sasa.

Comments