Timu Chelsea imeshindwa kuendelea na mbio za ushindi baada ya kukubali matokeo ya sare ya mabao 2-2 katika uwanja wa Liberty.
Chelsea ilipata bao la kuongoza kupitia Diego Costa aliyefunga dakika ya 18, hata hivyo kipindi cha pili Swansea ilichimoa bao kupitia Gylf Sirgusson aliyefunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 59.
Dakika 3 baadae baada ya bao la Sirgusson, Kiungo mholanzi Leroy Fer aliipatia Swansea bao la pili lakini Diego Costa kwa mara ya pili alirudi nyavuni na kuchomoa bao hilo dakika ya 81.
Ingawa Chelsea walishambulia kwa nguvu dakika za salama lakini Swansea walionekana kuwa watulivu na kuilazimisha chelsea sare ya mabao 2-2.
Kwa matokeo hayo kunaifanya Chelsea kukusanya jumla ya pointi 10 chini ya Manchester city yenye pointi 12 kwenye msimamo wa ligi kuu England.

Comments
Post a Comment