Tambwe arudi vizuri, Yanga ikiua 3-0


Timu ya Yanga imerejea kwenye hali ya ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea.

Mabao Yanga yamewekwa nyavuni na Donald Ngoma pamoja na Amis Tambwe aliyefunga bao mbili zilizotosha kuipa Yanga uhakika wa pointi 3.

Kwa matokeo hayo kunaifanya Yanga kukusanya idadi ya pointi 7, ikiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya JKT Ruvu.

Pia kesho katika uwanja wa Uhuru kutakuwa kati ya Simba na Mtibwa ambayo itachezwa majira ya saa 10 za jioni.

Comments