Tambwe, Ngoma waipaisha Yanga Shinyanga


Washabuliaji wa Yanga Amis Tambwe na Donald Ngoma wameendelea kufanya yao ligi kuu baada kutumbukiza nyavuni mabao pekee ya ushindi wa timu hiyo.

Yanga imeondoka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Mwadui ambapo Amis Tambwe alizamisha wavuni bao la kwanza na bao la pili lilifungwa na Donald Ngoma.

Tambwe na Ngoma wanandelea na kasi yao ufungaji kama ilivyokuwa msimu uliopita, na wiki moja kabla washambuliaji hao kwa pamoja walifunga katika mechi ya Ushindi dhidi ya Majimaji ya Songea.

Comments