TFF yakiri ubovu wa viwanja ni tatizo ligi kuu


Bodi ya ligi kuu TFF imekiri kuwepo kwa changamoto katika baadhi ya viwanja vinavyotumika katika mechi za ligi kuu ya Vodacom.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amekiri kuwa baadhi ya viwanja ni vibovu na havikidhi kutumika katika ligi.

Akitolea mfano wa Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga pamoja na CCM Kirumba wa Mwanza wambura aliongeza kuwa viwanja hivyo viwanja hivyo ni hatarishi kwa matumizi ya mechi za ligi kuu.

"Kweli zipo changamoto nyingi ambazo zinatukabili kwenye baadhi ya viwanja vinavyotumika ligi kuu, nadhani ipo haja ya kuangalia namna ya kutatua changamoto hizi." Alisema Wambura

"Nadhani unaweza hali halisi kutoka katika uwanja wa Kambarage pamoja na CCM Kirumba ni moja ya kati ya viwanja vibovu."  Alisema Wambura

Mbali na kauli hiyo ya mtendaji mkuu wa bodi hiyo pia makocha na wachezaji mbalimbali wamewahi kutoa malalamiko yao kuhusiana na matatizo ya viwanja hivyo.

Comments