Kamati ya Katiba, Hadhi na Sheria ya wachezaji imetoa siku 3 kwa timu ya Simba na Yanga kuanzia kuanzia Septemba 24 kumaliza suala la usajili wa mchezaji Hassan Kessy.
Kamati hiyo imefikia uamuzi baada ya kujadili kwa muda mrefu kesi hiyo ilyofunguliwa na Simba chini ya mwanasheria Richard Sinamtwa ambapo suala zima ni Kessy kusajiliwa na Yanga kabla mkataba wake haujafika kikomo.
Wakati huo mchezaji huyo anashikiliwa na Shitaka namba mbili ikiwa ni kushiriki mazoezi katika timu ya Yanga na kusafiri na timu hiyo nje ya nchi angali ana mkataba na Simba.
Edapo Simba na Yanga hawatafikia maridhiano ya suala hilo litarudishwa tena kwenye kamati na kutoa maamuzi kulingana na kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa.
Simba inataka kulipwa kiasi cha dola 600,000 kama sehemu ya fidia ambayo Yanga kutokana na kukiukwa kwa kanuni za usajili.

Comments
Post a Comment