Toto yaikaba koo African Lyon


Timu ya African Lyon ikiwa kwenye uwanja wa taifa leo imeshindwa kutamba mbele ya Toto Africa ya mwanza baada kutoka sare ya isiyokuwa na magori.

Mechi hiyo ilitawaliwa na utulivu wa hali ya juu katika vipindi vyote viwili vya mchezo huo na kuonesha uwezo unafanana katika eneo la kiungo.

Hata hivyo kipindi cha pili African Lyon walionekana kuchangamka kidogo baada ya kuingia kwa Peter Mwalyanzi ambaye aliongeza kasi ya mchezo kwa upande wa African Lyon.

Kwa upande wa African Lyon mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo Charles Otieno ameisifu Toto African kwa kiwango kizuri walichokionesha ugenini.

"Toto African wamecheza vizuri na wanastahili pongezi lakini kwa upande wetu tutajitahidi kufuta makosa yetu na kufanya vizuri kwenye mechi inayofata." Alisema Otieno.

Comments