Tshabalala wa Simba daladala ndo basi tena, akabidhiwa gari


Beki wa Simba Mohamed Hussein huenda akaachana rasmi na usafiri wa daladala baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari  aina ya Toyota Raum na mwenyekiti wa kamati ya usajili kwenye timu hiyo Zacharia Hans Poppe.

Tshabalala ambaye ameendelea kuwa na kiwango bora katika nafasi anayocheza uwanjani aliahidiwa zawadi hiyo endapo mchezaji huyo angeendelea katika kiwango alichonacho na hivyo mwenyekiti wa Simba ametimiza ahadi yake.

" Nimefurahi kupokea zawadi hii, nitajitahidi zaidi kujitoa na kupambana kwa ajili ya timu, nadhani hii nafasi yangu kuendelea na kiwango kwenye timu yangu." Alisema Tshabalala

Comments