Timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kufuzu kwenye michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) itajayofanyika nchini Gabon mwaka 2017 baada ya kuifunga Comoro bao 1-0.
Bao la Uganda lilifungwa na Farouk Miya na kuihakikishia safari ya moja kwa moja kwenye michuano hiyo The Cranes ambao wamekusanya jumla ya pointi 13.
Mara ya mwisho The Cranes ilishiriki mashindano hayo mwaka 1978 na sasa wamerejea tena wanarejea tena kwenye mashindano baada ya miaka 38 kupita.

Comments
Post a Comment