Wafahamu mabeki 10 bora wa kati wanaotikisa duniani kwa sasa

10. Ezequiel Garay 


Ingawa si maarufu duniani lakini mmoja kati ya beki bora duniani. Garay 29, anaichezea Zenit St Petersburg ya Urusi. Raia huyu wa Argentina amekuwa nguzo kwenye klabu yake na timu ya taifa, ana uwezo mkubwa kukaba na kucheza mipira ya juu kwa kichwa.

9. Gerard Pique 


Ingawa alishindwa kuwika Manchester united, kurudi kwake Barcelona mwaka 2009 kumeimarisha na kuinua kiwango chake. Gerard Pique amekuwa muhimili mkubwa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, ni mwepesi na mchezaji mwenye uwezo wa hali ya juu kutuliza na kumiliki mpira.

8. Pepe


Licha ya ukorofi na utovu wa nidhamu alionao lakini anaaminika kuwa mmoja kati  ya mabeki bora duniani, Pepe ana nguvu, anauwezo mkubwa kucheza mipira ya juu, na hufanya tackling nyingi uwanjani. Uwezo wake umefanya kudumu Real Madrid kwa muda mrefu akiingoza kubeba taji la klabu bingwa Ulaya mara 2.

7. Sergio Ramos


Pia ni mchezaji wa Real Madrid ambaye huambatana na Pepe kwenye safu ya ulinzi. Ana uwezo mkubwa wa kufunga kwa kichwa, amefunga magoli mengi kwa kichwa. Ramos ana nguvu, anauwezo mkubwa wa kumiliki mpira mguuni, na kufanya tackling. Beki huyu ni muhimili mkubwa kwa timu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania.

6. Gary Cahill 


Beki huyu alisajiliwa Chelsea mwaka 2012 akitokea Bolton. Ni beki mwenye uwezo wa hali ya juu uwanjani, Cahil anasifi wa kuwa moja kati ya mabeki bora wenye uwezo mkubwa wa kusambaza mpira kunako uwanja. Ana Nguvu, ana uwezo mkubwa wa kukaba pamoja kufunga kwa mipira ya kichwa. Ni moja kati ya mabeki wenye uwezo mkubwa wa kufanya tackling uwanjani.

5.Giorgio Chielini 

Beki huyu ambaye ni raia wa Italy alianza kucheza kama beki wa kushoto, ni moja kati ya mabeki wa kati wenye uwezo mkubwa uwanjani, ana pasi za uhakika uwanjani, ana nguvu, ana uwezo mkubwa kucheza mipira ya juu kwa kichwa na kufunga pia, Uwezo wake wa kukaba umemfanya kupata namba wakati wote katika klabu ya Juventus na taifa lake.

4. Vicent Company.


Raia huyu wa Ubelgiji alitua Manchester city mwaka 2008, Licha ya kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara lakini ana uwezo mkubwa kukaba, hakuna mshambuliaji wa England asiyefahamu shughuli ya kukatiza kwa beki huyu. Ana nguvu na umbo kubwa lililojengeka kimazoezi ambalo beki ana uwezo mkubwa wa kulifanyia kazi. Ni mzuri kwenye kufanya tackling na ana uwezo mkubwa kufunga na kuokoa mpira ya juu.

3. Thiago Silva


Moja kati ya mabeki bora duniani. Ni beki mwenye akili nyingi, mbinu na maarifa uwanjani. Thiago kwa muda mrefu amekuwa beki bora tangu alipokuwa Milan hadi sasa kwenye timu PSG.

2. Matt Hummels 



Ni beki aliyekulia kwenye akademi ya Bayern Munch na kuhamia Dortmund na sasa amerejea tena Bayern, beki huyu ana uwezo mkubwa wa kucheza mpira uwanjani, ni mwepesi ana akili na mbinu nyingi uwanjani. Unaweza kusema Hummels ametimia kila idara,

1. Diego Godin 


Raia huyu wa Uruguay hana kipingamizi kusimama kwenye nafasi hii kutokana na uwezo mkubwa alionao. Beki anamfanya Diego Simeon kujidai. Godin ni kiongoz mzuri wa ulinzi, ana akili nyingi, ana uwezo wa kufunga na kuokoa mipira mingi ya juu bila kusahau uwezo wake mkubwa wa kufanya tackling uwanjani. Bila shaka anastahili kuongoza kwenye orodha nzima ya mabeki.

Comments