West Ham yazidi kudidimia yachezea 3-0 kwa Southampton


Timu ya West Ham imeendelea kubaki mkiani ligi kuu England baada ya jana kukubali kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Southampton.

West Ham ilishindwa kutumia vema uwanja wake wa nyumbani na kuwafanya nyota wa Southampton Charlie Austin, Dusan Tadic na Ward-Prowse kukamilisha idadi ya pointi 3.

Hadi sasa West Ham imekusanya idadi ya pointi 3 pekee katika mechi 6 ilizocheza ambapo hadi sasa wamefungwa jumla ya magoli 16 ikiwa ndiyo timu iliyofungwa magoli mengi zaidi msimu huu.


Comments