Yanga yamnyima Omog usingizi


Kocha wa Simba Joseph Omog amesema kuwa licha ya timu yake kufanya vizuri kwa sasa lakini anawahofia zaidi Yanga ambao wanaonekana bado wapo imara.

Omog alisema kuwa Yanga wanaonekana kuwa wamejipanga, wachezaji wao ni imara, wana soka la kuvutia na wenye malengo huku wakionesha wazi nia yao ya kutetea taji la ligi kuu Vodacom.


"Yanga wako vizuri nadhani ni timu pekee ambayo inaninyima amani kwa sasa, soka lao ni la ushindani ukilinganisha na timu zingine." Alisema Omog.

Hadi sasa Simba ina mechi mbili mbele ikutane na Yanga, baada ya Azam na Majimaji mechi ya tatu itakuwa kati ya Simba na Yanga ambao kila mmoja anatamba kuwa bora msimu huu.

Comments