Kiungo wa Manchester city Yaya Toure amefuata nyayo za Didier Drobga baada ya kutangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa.
Yaya 33 alitangaza uamuzi huo kupitia tovuti yake baada ya kuitumikia Ivory Coast kwa miaka 12 na kuingoza kutwaa ubingwa wa kombe la mataifa Afrika mwaka 2015 wakati wote huo akiwa nahodha wa taifa hilo.
Toure alisema kuwa kwa sasa anahitaji kumpumzika kulingana na umri hivyo kwa upande wake anaona kuwa ni wakati sahihi kutandika daluga na kuwaachia vijana waongoze jahazi la tembo hao wa Afrika.
"Nimecheza kwa miaka 12 na kuiongoza timu ya yangu kubeba ubingwa mwaka 2015, nina miaka 33 sasa nadhani sitaweza kushiriki mazoezi kwa upande wa klabu na timu ya taifa, vijana wanastahili sasa kuchukua nafasi hii." Alisema Toure
Toure alianza kuitumika timu ya taifa ya Ivory Coast tangu mwaka 2004 na kuchukua nafasi ya unahodha iliyoachwa wazi na Didier Drogba mwaka 2014 baada ya Drogba kustaafu soka la kimataifa.

Comments
Post a Comment