Kocha wa timu ya Azam mhispania Zeben Hernandez amesema kuwa anakoshwa na jinsi timu yake inavyojituma na kupambana uwanjani baada ya kukusanya pointi 6 Mbeya.
Kocha huyo alisema kuwa hilo ndiyo jambo pekee ambalo ametaka wachezaji wake kufanya uwanjani huku akisisitiza kuwa Azam iko mbioni kuiva kama vile ambavyo yeye anataka.
"Wachezaji wananipa moyo na mbinu zangu zimeanza kuzaa matunda, nashukuru kwa kuwa wachezaji wanaonekana kunielewa tangu nilipowasili kwenye timu hii." Alisema Hernandez
"Mbali na mapungufu mbalimbali kwenye viwanja lakini wachezaji wamejitahidi kucheza vile ambavyo sisi makocha tulitaka ni jambo gumu kidogo hata hivyo imetupasa kubadilika kutokana na mazingira." Aliongeza kocha huyo
Kwa matokeo ya ushindi ambayo Azam ilipata jana dhidi ya Mbeya city kunaifanya timu kupaa juu ya msimamo wa ligi kuu na kuipiga chini Mbeya, pia Simba na Yanga ambazo zote zina mchezo mmoja mkononi.
SOURCE: www.azamfc.co.tz

Comments
Post a Comment