Aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Marekani Bob Bradley amekamata kibarua rasmi katika timu ya Swansea ya England baada ya kumwondoa aliyekuwa kocha wao Francesco Guidolin.
Bradley amewahi kuing'arisha Marekani katika michuano ya Mabara na kombe la dunia mwaka 2010 akiwa na nyota wa wakali kama Oguchi Onyewu, London Donovan, Clinton Dempsey na mwanae kipenzi David Bradley.
Swansea haijafanya vizuri tangu kuanza kwa ligi ya England msimu ikiwa na jumla ya pointi katika michezo 7 iliyocheza hadi sasa hali iliyopeleka uongoza wa timu hiyo kumwondoa Guidolin baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Liverpool.

Comments
Post a Comment