Uongozi wa timu ya Azam umesema kuwa hauna mpango wa kumtimua kocha wao Zeben Hernandez licha ya timu kuwa na mwenendo mbaya kwenye ligi.
Azam haijapata ushindi katika mechi sita ilizocheza mara mwisho ikiwemo sare nne ambazo timu hiyo imepata na kungufungwa michezo miwili.
Uongozi wa timu hiyo umeamua kumpa muda kocha huyo wakiamini kuna mazuri yanakuja ndani ya Azam chini ya Zeben Hernandez.
"Bado tunaimani na kocha wetu, tuna imani mambo mazuri yanakuja chini yake licha ya matokeo ambayo tumepata hadi sasa." Kilisema chanzo
Azam ina pointi 13 kwenye msimbamo wa ligi kuu ikiwa ikiwa imeachwa kwa pointi 13 na Simba anayeongoza msimamo wa ligi kwa pointi 26.

Comments
Post a Comment