Timu ya Azam itashuka dimba katika ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa leo katika uwanja wa Chamanzi Complex majira ya saa 1 usiku.
Azam kupitia msemaji wao Jaffar Idd wamesema kuwa wamejipanga vema na wako tayari kwa mchezo wa leo huku matumaini yao makubwa yakiwa ni kupata ushindi.
"Kwa upande wetu tuko sawa nadhani hakuna tatizo, tumejipanga vizuri na mechi ya leo." Alisema Idd
Kwa upande mwingine msemaji huyo alisema kuwa wachezaji waliokuwa kwenye majeraha akiwemo Pascal Wawa na Erasto Nyoni wako fiti na wamerejea uwanjani kwa ajili ya mechi ya leo.
"Wachezaji wetu waliokuwa majeruhi akiwemo Pascal Wawa na Erasto Nyoni wamerejea uwanjani na wapo tayari kuikabili Ruvu Shooting."

Comments
Post a Comment